Posts

Showing posts with the label BURUDANI

Kisa Pombe, Mkude Akalia Kuti Kavu Simba

Image
HALI ya mambo huenda isiwe poa tena kwa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkode kutokana na tukio analodaiwa kulifanya hivi karibuni wakati timu hiyo ilipokuwa ikisafiri kwenda Kanda ya Ziwa kucheza mechi za Ligi Kuu Bara.
Mkude hakusafiri na timu hiyo baada ya kudaiwa kuachwa na ndege ikielezwa alipitiwa na usingizi katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa imeweka kambi. Hata hivyo, habari ambazo Championi Ijumaa limezipata kutoka ndani ya Simba zimedai kilichosababisha Mkude aachwe ni pombe kwani alienda nyumbani na kila alipokuwa akipigiwa simu akawa hapokei.
“Kwa hiyo kesho (leo) uongozi utaweka wazi hatua ambazo utamchukulia kutokana na kosa hilo alilofanya ambalo kusema kweli si la kiungwana,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Suala lake kwa sasa lipo kwa uongozi wa juu na siyo kwa kocha tena kwani, kocha yeye anataka nidhamu katika kikosi chake na ameshatoa msimamo wake kwa uongozi kuhusiana na Mkude, hivyo kesho (jana) ndiyo tutajua hatima yake.” Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Kocha Mk…

Kuna wakati Ebitoke alilia mwenyewe!

Image
UNAFIKIRI kupanda Mlima Kilimanjaro ni kazi lelemama? Sasa taarifa ikufikie kuwa komediani mkali Bongo, Annastazia Exvery ‘Ebitoke’, amejikuta akilia peke yake baada ya kuona uzalendo unataka kumshinda wakati akipanda Mlima Kilimanjaro wikiendi iliyopita.
Ebitoke ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, wakati akipanda na wenzake, ulifika wakati akaona hawezi tena kutembea ndipo akaona kuliko kushindwa, ajikaze hivyohivyo huku machozi yakimtoka.
“Kupanda Mlima Kilimanjaro ni raha na ni ushujaa, lakini lazima uchanganyikiwe kwanza, maana sikutaka kupitwa, lakini nilipoona nataka kushindwa nililia kama mtoto kisha nikafuta machozi na safari ikaendelea,” alisema Ebitoke aliyekuwa kwenye msafara wa mastaa kibao waliopanda Mlima Kilimanjaro wikiendi iliyopita.

Harmonize Apiga Bao Lingine!

Image
DAR ES SAAAM: Staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ anaendelea kung’ara kila kona na sasa amepiga bao lingine la kimataifa. Harmonize au Harmo, wiki hii ameng’ara tena baada ya kutajwa kama mwanamuziki pekee kutoka Afrika Mashariki atakayewania tuzo kubwa za muziki barani Ulaya za MTV Europe Music Awards kwa mwaka 2019. Mwaka 2019 vipengele vya Tuzo za MTV Europe Music Awards vimetangazwa na zitafanyika Novemba 3, 2019 jijini London nchini Uingereza ambapo Harmo anashindanishwa na wanamuziki kutoka Afrika Magharibi. Mbali na Harmo, wanamuziki wengine wanaowania tuzo hiyo kwenye Kipengele cha Best African Act 2019 ni Burna Boy, Teni, Nasty C, Prince Kaybee na Toofan. Akizungumzia ishu hiyo, meneja wa Harmo; Beauty Mmary ‘Mjerumani’ alisema ni nafasi nyingine kwa mwanamuziki huyo kung’aa kimataifa na kuwaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti kwa kumpigia kura kwa wingi ili alete ushindi Bongo.
“Ni jambo kubwa, tunaomba mashabiki na watu wote wanaopenda muziki huu ufike mbali…

Diamond aibua mjadala kuoa wake 3!

Image
DAR ES SALAAM: Kumewaka moto! Muda mfupi baada ya tetesi kusambaa mitandaoni kuwa staa grade one kunako Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ana mpango wa kuoa wake watatu, ameibua mjadala matata, Gazeti la Ijumaa limedokezwa!
Hivi karibuni Diamond au Mondi anayetikisa kila kona na Wimbo wa Yope Remix akiwa ameshirikishwa na mwanamuziki Innocent Balume ‘Innoss’B’ mwenye asili ya Kongo DR, alikaririwa akisema licha ya kuwa na mpenzi ambaye ni mtangazaji wa redio mwenye uraia wa Kenya; Tanasha Donna, matumaini yake ni kuoa wanawake wawili au watatu mbele.
Staa huyo ambaye ni mmiliki wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) aliwahi pia kuulizwa kuhusu kuonekana katika picha akiwa na warembo tofautitofauti kwenye hoteli mara kwa mara na kusema;
“Siyo kwamba napiga picha na warembo wa mjini hotelini mara kwa mara. Simba (mnyama) ukimuona ana ubora mkubwa, anaweza kuwa na wake wawili au watatu, lakini linapokuja suala la kumgusa tu umekwisha.” Kauli hizo zimeibua mjadala mkubwa ndani na…

Kwa Nini LYNN Asilindwe?

Image
BAADA ya minong’ono ya hapa na pale kumhusu msanii wa Bongo Fleva, Irene Louis ‘Lynn’ kutinga na mabaunsa wanne kwenye sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika Dunken House maeneo ya Mikocheni, Dar, mwenyewe amesema alifanya hivyo kutokana na uzuri alionao.
Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa, Lynn alisema watu wanaona kitu gani cha ajabu yeye kulindwa na mabaunsa kwani ni jambo la kawaida ukizingatia yeye ni msichana mrembo anayetakiwa kulindwa siku zote.
“Watu wanashangaa kwa nini ninalindwa na mabaunsa? Kwani hawajui mimi ni msichana mrembo ninayestahili kulindwa? Mimi nitalindwa wakati wowote,” alisema Lynn aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Mondi’.

Kuhusu Sister FEY na Penzi Lake Kwa Diamond Platnumz..

Image
Sister Fay amesema kuwa kama angekuwa hajaolewa basi msanii wa BongoFleva ambaye angetamani amuoe ni Diamond Platinumz kwa maelezo kuwa Mond ni moja ya wanaume wapambanaji .
.
Aidha, Sister Fey amesema hapendi mambo ya kiki kwasasa kwa madai mumewe amerudi Bongo

50 Cent adai Chris Brown ana uwezo mkubwa kimuziki kuliko Michael Jackson

Image
Msanii 50 Cent bado anaendelea kusimamia msimamo wake kuwa Chris Brown ni mkali zaidi ya Michael Jackson.

Siku ya jana mchanaji huyo alichapisha video mtandaoni akiwa anatumbuiza kwenye moja ya show zake za hivi karibuni na kummwagia sifa za kutosha Chris Brown.
Loading...
“Kama ningekuwa nafanya R&B basi nisingefurahia, huyu Jamaa Chris Brown ni Mkali sana zaidi ya Michael Jackson” 50 Cent alieleza.

 Agosti mwaka huu aliibuka na kummwagia sifa kama hizo Chiris Brown baada ya kufikisha idadi ya Mauzo Million 70 ya ngoma zake kwa Marekani tu.

Tiwa Savage afunguka mahusiano yake na Wizkid

Image
Msanii maarufu wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage amefunguka kuwa kwasasa bado yupo single hajapata mwanaume wa kuishi naye tangu aachane na mumewe,  Tee Billz  mwaka 2016.

Loading...

Akihojiwa jana asubuhi na kituo cha radio cha The Beat 99.9 cha Jijini Lagos, Nigeria. Tiwa Savage  amesema hajawahi kuwa kwenye mapenzi na mwanaume yeyote tangu aachane na mumewe na wanaume wote anaoonekana nao ni marafiki wa kibiashara tu.

Kuhusu tetesi za kuwa anatoka kimapenzi na Wizkid, Tiwa amesema kuwa ‘Mimi na Wizkid ni marafiki wa kibiashara tu”, Na akaendelea kujibu kuhusu mustakabali wa mahusiano yake mapya kwa sasa.

“Bado nipo single kwasasa na hakuna hata mwanaume anayenitafuta DM“, amefunguka mrembo Tiwa Savage na kukazia kuwa kwasasa yupo bize na kazi yake ya muziki.

SOMA ZAIDI KISA CHA TIWA SAVAGE KUACHANA NA MUMEWE MWAKA 2016.

Mwaka 2016 kwenye exclusive interview na Pulse TV, Tiwa alisimulia jinsi ambavyo mume wake alikuwa akimfanyia ikiwa pamoja na kumtelekeza kwa kutotaka kujua chochote…

Baada ya Kujitoa WCB Sasa Harmonize na Zari Mambo Motomoto

Image
YAPATA zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu ilipofahamika rasmi kwamba, supastaa wa Bongo Fleva; Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’, amejitoa kwenye lebo ya muziki iliyomlea ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya mwanamuziki Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.

Hata hivyo, tukio hilo lingali bado linatrendi, kuna mengi nyuma yake huku kila mtu akisema lake, lakini kubwa ni ukaribu motomoto ulioibuka kati ya Harmonize au Harmo na eksi wa Diamond au Mondi; Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Loading...
ZARI DUBAI
Akiwa Dubai kwenye bata ndefu wakati wa birthday yake mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari alirekodiwa kipande cha video akiimba na kucheza wimbo mpya wa Harmo wa Inabana alioshirikiana na mwanamuziki wa Uganda, Eddy Kenzo.
Si unajua tena zile mbwembwe za Zari? Yaani tukio kubwa la birthday ya mama watano lipite hivihivi bila kujulikana?

ATUPIA NUSU UTUPU
Basi unaambiwa akiwa kule Dubai ndipo akawa anafanya mambo kibao ya kusababisha vichwa vya habari kama kukaa na kutupia nusu utupu kis…

Sawa Tumekubali Harmonize Atapotea...JE WCB ina Uwezo wa Kumtengeneza Harmonize Mwingine?

Image
Moja ya mijadala mingi iliyoko mitandaoni ni kuhusu Harmonize kujiondoa Kwenye lebo yake ya WCB,Ukifuatilia comment za mijadala hiyo wengi mashabiki wa Diamond platnumz (WCB) wanadai huo ndo mwisho wa Harmonize,in short atapotea kwenye game,Hilo hatuwez kubishana nalo coz ndo mfumo wa mziki wetu kuwa mikonon mwa baadhi ya watu.

Ila swali Langu ni je,WCB wana uwezo na nguvu tena ya kumtengeneza Harmonize mwingine?

Nakumbuka miaka kadhaa nyuma kuna lebo ilikuwa inajigamba kumtengeneza JAYZ na kumfikisha pale alipo,Siku moja Jayz akiwa anahojiwa na kituo kimoja aliulizwa kuhusu Hao watu wanao jigamba kumtengeneza yeye,Jayz aliwajibu "Kama ni rahisi kumtengeneza Jayz Basi wamtengeneze Jayz mwingine"

Swali Langu bado ni lile lile,Je WCB wanao uwezo tena wa kumtengeneza msanii wa levo ya Harmonize? Mana kwa wasanii walioko pale WCB hakuna wakufika Hata nusu ya Levo ya Harmonize ukimwondoa Diamond.

Mwana FA Aweka Rekodi Mpya, Msanii Wa Kwanza Tanzania

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Mwana FA ameweka rekodi mpya baada ya kufanikiwa kufika Kilele cha Uhuru Cha mlima Kilimanjaro na kuwa msanii wa Kwanza Tanzania kufika kileleni miongoni mwa walioshiriki kampeni iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla.

Mwanafa pamoja na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya na Bongo Movies wameshiriki katika challenge ya kupanda Mlima huo ikipewa jina la HK Kilimanjaro Challenge 2019.

Hapa Ndipo Wanaume Wengi Wanafeli Kwenye Kumuingiza Dem Box

Image
Kutongoza/kumuingiza mwanamke Box kuna kanuni zake kama ilivyo kanuni za kufanya hesabu, maana usipokuwa makini kujua kanuni za kufanya  hesabu ni lazima tu hesabu hiyo utakosa. Hivyo hivyo hata katika mapenzi kama hujui namna ya  sahihi ya kumtongoza mwanamke ni lazima mwanamke huyo utamkosa tu.

Haya ndyo yanayofanya Wanaume wanafeli

1.Kuwa na papara.
Wanaume wengi wamekuwa na haraka sana tunapokuwa tukitaka kuaproach hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu. mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake. Mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata kwa sababu atakufikiria sana juu ya uharaka wako.

2.Kuonyesha maisha yasiyo ya uhalisia.

Wanaume wengi wamekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu. Unaaproach jaribu kuwa real. huwezi kumwambia mdada unafanya kazi benki  wakati si kweli.

3.Kutokusoma Mood ya mwanamke.
Unapomuaproach wanamke lazma usome mood yake coz sometime unaweza kutoswa coz hujamsoma mwanamke.unamtongozaje mwanamke asubuhi?,,

4.…

Njia 16 Muhimu Za Kuondoa Sumu Mwilini Kwa Kutumia

Image
Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.

Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini:

1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee
Amua moja ya mlo wako kwa siku uwe ni matunda pekee bila chakula kingine zaidi. Unaweza kuamua ama chakula cha asubuhi au cha jioni kuwa ni matunda pekee, ndiyo kwenye sahani yako unajaza matunda tu mbalimbali sahani ijae na ule hayo tu kama ndiyo mlo wako ukimaliza unaweza kunywa juisi ya matunda au maji pekee.

2. Kula vyakula vya asili zaidi kuliko vya viwandani
Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi k…