Posts

Showing posts with the label MICHEZO

Bao Aliofunga Makame ni shangwe tupu Yanga

Image
Dar es Salaam. Bao la Abdulaziz Makame katika dakika ya 51, limetosha kuipa Yanga ushindi wa kwanza msimu huu wakichapa Coastal Union 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Bao hilo la utata lililofungwa na Makame limeiwezesha Yanga kupata pointi tatu na kufikisha pointi nne katika mechi tatu za Ligi Kuu Tanzania walizocheza hadi sasa. Makame wiki iliyopita aliacha simanzi Yanga baada ya kujifunga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zesco, lakini leo ameibuka shujaa kwa kufunga goli hilo pekee. Makame ameandika bao hilo baada ya kuunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na beki Ali Ali ambaye awali aliunganisha kona iliyopigwa na Mrisho Ngassa kabla ya Makame kuugonga na wakati beki wa Coastal Union akijalibu kuokoa uligonga mwamba na kudunda ndani ya mstari na mwamuzi kuamua bao. Mwamuzi, Abubakar Mturo kutoka Lindi alilaumiwa kutokana kushindwa kuwa na mawasiliano mazuri na wenzake. Utata wa Mwamuzi huyo ulimfanya kushindwa kutoa uamuzi ya haraka katika bao lililofungwa na Ya…

Hivi Mkude anaonewa au kuionea Msimbazi?

Image
In Summary Wapo wanaoamini Mkude amefanya kosa na anapaswa kuadhibiwa, pia kuna wanaodhani kiungo huyo amekuwa hatendewi haki ndani ya Simba na tuhuma hizo zinalenga kumchafua. Dar es Salaam. Kiungo Jonas Mkude yupo kikaangoni kwenye kikosi cha Simba kwa sasa baada ya kushindwa kusafiri na timu hiyo kwenda Kanda ya Ziwa wiki iliyopita ambako timu hiyo ilicheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Biashara United.
Nahodha huyo wa zamani wa Simba, alikacha safari hiyo pasipo ruhusa, pia uongozi na timu kutokuwa na taarifa yoyote juu ya kutosafiri kwake.
Hata hivyo, habari za ndani zinadai Mkude hakuwepo kambini wakati msafara wa timu ulipokuwa unaondoka kwenda uwanja wa ndege jambo lililofanya aachwe.
Wakati uongozi wa Simba ukidaiwa kuwa mbioni kumpa adhabu kiungo huyo, mitazamo na hisia za wapenzi na mashabiki wa soka imetofautiana.
Wapo wanaoamini Mkude amefanya kosa na anapaswa kuadhibiwa, pia kuna wanaodhani kiungo huyo amekuwa hatendewi haki ndani ya Simba na tuhuma hizo zinalenga…

Samatta Ashusha Pumzi

Image
BAADA ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Napoli ya Italia kwenye uwanja wao wa nyumbani, nahodha wa KRC Genk na Taifa Stars, Mbwana Samatta amefunguka kuwa kitendo cha kutoka 0-0 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwao ilikuwa ni nafuu kuliko kipigo ambacho walipata awali dhidi ya RB Salzburg.
Genk, juzi Jumatano ilishindwa kutamba kwenye Uwanja wa Luminus baada ya mchezo wa kwanza Hatua ya Makundi kufungwa mabao 6-2 na Salzburg.
“Tumecheza dhidi ya Napoli ambao ni wagumu kweli, lakini tulipambana na hatujapata matokeo mabaya kama ambavyo ilikuwa kwa Salzburg.
“Ilikuwa muhimu kwetu kupata sare kwenye ligi hii, tulipata nafasi hatukutumia vizuri, nao kwao ilikuwa hivyohivyo,” alisema Samatta. Msimamo kamili wa makundi ya Uefa soma ukurasa wa 18.

Yanga Wamletea Ubishi Mo

Image
YANGA ni kama wanamletea ubishi mwekezaji wa Simba, bilionea, Mohamed Dewji ‘Mo’, hiyo ni baada ya kutangaza miezi minne sawa na siku 120 za kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Kaunda uliopo kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani, Dar.

Hatua hiyo imekuja siku chache tangu Mo atembelee Uwanja wa Bunju unaomilikiwa na Simba ambao upo kwenye hatua za mwisho za kukamilika hasa ule wa mazoezi upande wa nyasi bandia. Mara baada ya Mo kutembelea uwanja huo aliahidi kumalizika kwa uwanja huo hivi karibuni kutokana na nyasi bandia kutua nchini na kupelekwa uwanjani hapo tayari kwa kuwekwa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa hadi kufikia Februari 2020 ukarabati wa uwanja huo utakuwa umekamilika.
Mwakalebela alisema kuwa uwanja wamepanga kuutumia kwa ajili ya mazoezi, pia kambi ya pamoja ya kikosi chao katika kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara na kimataifa.
Aliongeza kuwa hivi karibuni wanatarajia kuanza ukarabati wa jengo l…

Winga wa Juventus Douglas Costa Ampongeza mchezaji wa Simba

Image
Winga wa Juventus Douglas Costa Ampongeza mchezaji wa Simba
Winga wa miamba ya soka nchini Italia klabu ya Juventus, Douglas Costa amempongeza mchezaji wa Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC, Fraga Vieira kwa kuongeza mwaka mwingine katika siku yake ya kuzaliwa.

Loading... Kupitia akaunti yake ya Instagram, Douglas Costa amemtumia ujumbe mfupi beki huyo Simba baada ya kuweka picha yake ambayo akionekana akimwagiwa maji na wachezaji wenzake wa Msimbazi.

Douglas Costa de Souza akiwa na Ronaldo

Douglas Costa de Souza amempongeza nyota huyo kwa kuandika kuwa ”Caraleo, umekuwa 👴 !  nakumbuka ukiwa chini ya miaka -15 Gerson 😂😂😂 hongera shujaa,”  amesema mchezaji huyo wa Juventus.


Fraga Vieira raia wa Brazil amesajiliwa Simba SC akitokea katika klabu ya ATK FC ya India kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo mwenye ambaye sasa anatimiza miaka 27 ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji.

Vieira amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Brazil ya vijana we…

Ole Gunnar Anaamini Akimsajili Huyu Toka Barcelona Ataifufua Man U

Image
Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kama sehemu ya kufufua kikosi cha Manchester United. Pia wanaendelea kumfuatilia kiungo wa klabu ya Leicester na timu ya taifa ya England James Maddison, 22, ambapo wanaweza kumsajili kwa pauni milioni 80.

Suarez Aikoa Barcelona Na Majanga Ya Inter Milan

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez anayeichezea FC Barcelona ya Hispania usiku wa October 2019 katika uwanja wa Nou Camp aliibuka shujaa wa mchezo dhidi ya Inter Milan wa UEFA Champions League hatua ya makundi baada ya mchezo wao wa kwanza kutoka sare ya 0-0  dhidi ya Borussia Dortmund. Barcelona baada ya kurudi katika uwanja wao wa Nou Camp walianza vibaya kwa kujikuta wakiruhusu kufungwa goli la mapema na Inter Milan dakika ya pili kupitia kwa Lautaro Martinez lakini mambo hayakuwa mazuri kwa Barcelona hadi walivyoingia kipindi cha pili. Luis Suarez ndio alikuwa mkuki wa sumu wa Inter Milan kwani alifunga goli la kusawazisha dakika ya 58 na kufunga goli la ushindi dakika ya 85 na kuufanya mchezo umalizike kwa Barcelona kupata ushindi wa 2-1, Lionel Messi akiibuka kidedea kwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi (6) kuliko mchezaji yoyote katika mchezo huo, Barcelona sasa wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point 4 katika kundi lao sawa na Dortmund ayeongoza wakati Inter Milan na…

CR7 Aweka Rekodi Mpya Juventus

Image
Cristiano Ronaldo ameweka rekodi nyingine ya ufungaji katika Ligi ya Mabingwa baada ya kufunga dhidi ya Bayer Leverkusen usiku wa Oct 1.
Ronaldo alifunga bao dakika 88, katika ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Juventus katika mchezo wa Kundi D uliofanyika kwenye Uwanja Allianz.
Bao hilo la Ronaldo linamfanya nyota huyo kufunga dhidi ya timu 33 katika Ligi ya Mabingwa akifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Raul.
Ronaldo haiwezi kujisahau kwa rekodi hiyo kwa sababu mshindani wake mkubwa Lionel Messi naye amezifunga timu 32 katika mashindano hayo.

Rio Fernando Amtaka Kane Afungashe Virago

Image
Rio Ferdinand amezidi kumsisitizia straika Harry Kane kwamba akusanye virago vyake na kuachana na Tottenham Hotspur kwa sababu inampotezea tu wakati.
Beki huyo wa zamani wa Manchester United, Rio amemtaka Kane kuachana na Spurs ili kwenda kujiunga na timu itakayompa fursa ya kubeba mataji kama yeye alipofanya hivyo alipoachana na Leeds United.
Kane hajashinda taji lolote kubwa tangu alipojiunga na Spurs ambapo msimu uliopita kikosi hicho kilichapwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mara ya mwisho, Spurs kubeba taji ilikuwa mwaka 2008 wakati walipowapiga Chelsea kwenye fainali ya Kombe la Ligi.
Na Ferdinand anamwambia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuachana na Spurs kabla muda haujamtupa mkono.

Mbwana Sammata Dimbani Tena Leo, Atafanikiwa Kufanya Unyama?

Image
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa leo akiwa na klabu yake ya KRC Genk anatarajiwa kushuka dimbani kwa mchezo wake wa pili wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (Champions League) dhidi ya Napoli. Genk, itakuwa nyumbani Ubelgiji katika dimba la Luminus Arena ikiwakaribisha miamba kutoka Italia klabu ya Napoli. Katika mchezo wake wa kwanza Genk iliangushiwa kichapo kizito cha goli 6-2 ugenini dhidi ya RB Salzburg, huku Samatta akifunga goli moja la kufutia machozi.
Katika mchezo huo, Samatta aliweka rekodi binafsi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Champions League na kufunga goli.

Neymar Athibitisha Yeye Na PSG ni Damu Damu, Haendi Mahali

Image
Neymar aliyekuwa akiwaniwa na Barcelona na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu, ameibuka na kauli ya kuwafurahisha mashabiki akisema hana mpango wa kuondoka PSG.
"Nina furaha ninapokuwa uwanjani na kuisaidia PSG kufanya vizuri, ni jambo zuri pamoja na mashabiki wetu," alisema.
"Hii ni kama vile unapokuwa na mchumba wako, kuna wakati unakua mbaya kwenu, lakini kumbatio na mapenzi ya dhati inakuwa vizuri," alisema Neymar.
Neymar aliongeza anataka maisha yake yawe PSG, na anataka kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kutwaa mataji zaidi.

Maneno Ya Kujitete Ya Kocha Wa Man United

Image
Ole Gunnar Solskjaer anasisitiza kwamba yeye ni mtu sahihi wa kuiongoza Manchester United, licha ya kwamba timu yake ipo alama tatu tu juu ya mstari wa kushuka daraja. Tangu Solskjaer apewe rasmi usukani wa kuinoa klabu hiyo mwezi Machi, Man United wameshinda mara tano tu katika mechi 18. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, anapigiwa upatu kuwa miongoni mwa makocha wawili wa ligi ya Primia waliopo kwenye hatari ya kupoteza ajira zao muda wowote pamoja Marco Silva wa Everton . "Mimi mwenyewe sina wasiwasi, kama sitajiamini mwenyewe basi dunia yote itakosa imani nami" amesema kocha huyo. United inatarajia kucheza na Arsenal usiku wa leo baada ya kupoteza mechi ya nyumbani dhidi ya Crystal Palace na ugenini dhidi ya West Ham katika msimu huu. Klabu ipo nyuma ya vinara Liverpool kwa pointi 13 na kuwa na pointi tatu tu mbele ya Aston Villa iliyopo nafasi ya 18, ambayo ndipo mstari wa kushuka daraja huchorwa. "Tulikuwa na mjadala mkubwa sana, lakini tunaamini kile tunachokifanya,&q…