Posts

Showing posts with the label NEWS

LIVE: Ziara ya Rais Magufuli Tunduma – Songwe

Image
Rais Dk. John Magufuli leo Oktoba 5, 2019 amezindua ujenzi wa barabara ya Mpemba – Isongole iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 50.3 ambayo imegharimu Tsh bil 109.439, ujenzi utakamilika mwaka 2020. Magufuli pia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Tunduma mkoani humo. “Niwaombe wananchi muendelee kufuata sheria, ukijenga kwenye hifadhi ya barabara tutabomoa tu, walisema ghorofa la TANESCO Ubungo halitabomolewa, nimeingia madarakani nimelibomoa.”
“Mkandarasi kutoka China anajenga kilometa 50 kwa miaka mitatu? Hii ni kwasababu wasimamizi wetu wa Wizara wanazungumza naye kwa raha, najua Waziri umenielewa, hizi fedha za miradi zinatoka kwa Watanzania masikini na huu ni mtego kwako.” “Miradi mikubwa tunayoifanya nchini na ununuzi wa ndege ni matokeo ya kupambana na rushwa.” Rais Magufuli akiwa ziarani Wilayani Mbozi mkoani Songwe,” amesema Magufuli.
“Mh Rais kinachosababisha Ileje isiendelee zaidi ni Mkurugenzi wetu…

Aliyekiri Kuhujumu Uchumi Ahukumiwa Jela, Faini Sh mil 100 – Video

Image
MFANYABIASHARA Yasin Katare amehukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulipa faini ya Mil.100 au kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri mashitaka ya utakatishaji fedha. Mshitakiwa Katare yupo katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) Godfrey Gugai ambao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi. Adhabu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo wakili wa utetezi, Shunde Mbutu aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mshitakiwa kwa sababu ni kosa lake la kwanza. Pia amedai kuwa ana familia inayomtegemea, amedai amekaa ndani mwaka wa pili na afya yake si nzuru kwani anaumwa na amekuwa akienda Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhudhuria kliniki. Hakimu Simba amemuhukumu mshitakiwa kulipa faini ya Sh.Mil 100 kwa kuzingatia muda aliokaa gerezani muda mrefu na ni mgonjwa hivyo, wakimpa adhabu kubwa itaendelea kutesa familia yake. Pia amesema, nyumba ya mshtakiwa itatai…

Rais Magufuli Amwagia Sifa RC wa Mbeya Aliyewai PA Viboko Wanafunzi Asema Nilimwagizala Kuwatimua Wanafunzi

Image
RAIS  John Magufuli amesema alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kuwafukuza shule wanafunzi wote wa kidato cha tano na sita wa Shule ya Sekondari Kiwanja iliyopo Chunya na kuivunja bodi ya shule hiyo baada ya wanafunzi hao kukamatwa na simu za mkononi na kuchoma moto mabweni Oktoba 1, 2019.


Loading...
Magufuli amesema hayo leo Ijumaa, Oktoba 4, 2019, wakati akizungumza na wananchi wa Songwe katika ziara yake ya siku nne, mkoani humo ambayo ameianza leo.


“Nampongeza RC wa Mbeya (Chalamila), kwa wale watoto waliotimuliwa shuleni lazima wazazi wao walipe. Nasema haya si kwamba sina huruma, nimeshawahi kuwa mwalimu, nafikiri kuna mahali tumekosea hii sheria kuhusu viboko.“Baba wa Taifa aliwazungumzia maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini na bado hawajabadilika, hawa ni maadui wakubwa katika maendeleo yetu.  Kila awamu ilijaribu,  na awamu hii pia bado inajitahidi kukabiliana na hao maadui.“Naagiza uongozi wa Jimbo la Mbozi, kuacha mara moja kuchangisha wananchi mi…

Waziri Mkuu Akagua Mradi Wa Maji Manyoni....Unatarajiwa Kugharimu Zaidi Ya Sh. Bilioni 10

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa mradi wa maji wa Kintiku – Lusilile ulioko Manyoni ambao awamu yake ya kwanza inatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 22, mwaka huu.

Akizungumza na watumishi na wakadarasi leo (Ijumaa, Oktoba 4, 2019) mara baada ya kukagua mradi huo akiwa njiani kuelekea Manyoni, Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi huo pamoja na kasi ya mkandarasi.
Loading...
Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Singida, alielezwa kwamba mradi huo utahudumia vijiji 11 vya Kintinku, Lusilile, Maweni, Mvumi, Ngaiti, Chikuyu, Mwiboo, Mbwasa, Mtiwe, Makutupora na Chilejeho ambavyo viko kando ya barabara kuu itokayo Singida kwenda Dodoma.

Akitoa taarifa ya mradi mbele ya Waziri Mkuu, Meneja wa RUWASA, Injinia Gabriel Ngongi alisema wananchi zaidi ya 55,000 watanufaika na mradi huo pindi utakapokamilika. Alisema awamu ya kwanza imegharimu sh. bilioni 2.46.

Akizungumzia halia halisi ya utekelezaji wa mradi huo, alisema ujenzi wa tenki la kuhifadhia maj…

Jibu la chadema kwa msajili wa vyama lawekwa bayana

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekanusha kukiuka sheria ya vyama vya siasa kama ambavyo barua kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa nchini inavyoeleza.

Loading... Kupitia taarifa iliyotolewa leo Oktoba 3, 2019 na mkuu wa idara ya mawasiliano ya chama hicho Tumaini Makene, chama kimekiri kupokea taarifa hiyo lakini wamesema Katiba ya chama hicho inatoa mamlaka kwa kamati, kusogeza mbele uchaguzi mkuu ndani ya chama.


” Tarehe ya uchaguzi mkuu wa chama, inaweza kurekabishwa kwa kusogezwa mbele kwa muda usiozidi mwaka mmoja, toka mwisho wa uhalali wa uongozi uliopo, mamlaka ya kufanya marekebisho haya yameachwa kwa kamati kuu” imeeleza taarifa hiyo.

Kwamujibu wa taarifa hiyo, Kamati kuu ya chama hicho, ilikaa katika kikao chake cha tarehe 27 na 28, Julai, 2019 na kurekebisha ratiba ya uchaguzi, ambapo utakamilika mwezi Disemba kwa ngazi ya taifa na kwamba kwasasa kinaifanyia kazi barua hiyo ili iweze kuifikia Ofisi ya msajili wa vyama vya Siasa ndani ya muda husika.


Awali ofis…

Nikupongeze Mh Rais kwa Kuungana na RC Chalamila

Image
Habarini za asubuhi wanajamvi...
Loading...
Hakika kutoka ndani ya moyo wangu naomba kumpongeza Mh Rais kwa kwenda sambamba na RC Chalamila kuwachapa viboko wanafunzi waliochoma bweni kisa wamenyang'nywa simu..

Kwanza kuwa na simu ili hali wewe ni mwanafunzi ni kosa la kwanza na kuchoma bweni ni kosa la pili,

Kabla Mh Rais hajampongeza RC Chalamila Mimi nilimpongeza kimoyomoyo,kizazi cha sasa cha hovyo sana,tusipoenda nao kwa style hii walimu watapata tabu sana,

Kitu ambacho vijana hawa bado hawajakielewa Nchi imebadilika sana,wasifikiri tupo awamu ya nne ya mchezo mchezo hii ni awamu ya tano ya kazi tu hatuna muda na mambo ya kijinga kama haya eti unachoma bweni kisa kunyang'anywa simu wakati tayari umevunja sheria kumiliki simu shuleni?Nakupongeza sana Mh Rais kwa kuliunga mkono hili,

Tukiendelea kulea mambo ya kijinga kama haya tutashindwa kupiga hatua...

Hongera Mh Rais

Hongera RC Chalamila

By Huko Kwenu Vipi/JF

Adhabu ya Viboko ilijenga Taifa Lenye Nidhamu kuanzia Mashuleni Mpaka Majumbani !

Image
Nakumbuka kipindi kile cha shule ya msingi tulikuwa na mwalimu anaitwa Mr Kitunga ukiambiwa unaenda kuoga fimbo zake mikojo inakutoka kabla ya kufika kwenye adhabu yenyewe na ukifika shule tayari watu wapo mstarini ni vyema urudi hospitali kwenda kuchukua cheti cha dokta uzuge unaumwa

Loading... Hali ile ilijenga nidhamu ya hali ya juu na kutochelewa shule na ndio watu waliitumia kujenga nidhamu na uwajibikaji mpaka makazini

Lakini kilipokuja hiki kizazi cha laktojeni na vyama vingi vya siasa kila kitu kimebadilika, taifa limekuwa na vijana wa hovyo wa kuvaa kata K. Hata ukimtuma mtoto wa jirani anakukatalia bila soni.

Toto halijawahi kupigwa hata kibao akiadhibiwa na mzazi wake basi ni kwa njiti ya chelewa,matokeo yake ndio hawa wanaona Rais John Magufuli kila alifanyalo anawaonea hawawezi kuwajibika wala hawana nidhamu wala uzalendo mwisho wa siku anafikia kuchoma shule moto.

Ni vyema sasa ifikiriwe kurudisha adhabu ya viboko ili watoto wanyooke tuondoe taifa legelege,nidhamu ichukue mk…

Askari 6 Akiwemo wa JWTZ Wakuhumiwa kwa Wizi wa Mafuta ya Ndege

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu askari sita akiwemo Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja bada ya kukiri shtaka la wizi wa mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik).

Loading...

Askari hao ni Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo baada ya Washtakiwa hao kukiri shtaka linalowakabili.Mwaikambo alisema kwa kuwa Washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza hivyo mahakama hiyo imewapa adhabu ya kulipa faini hiyo kila mmoja na madumu 109 yenye mafuta hayo yatarudishwa serikalini.Awali wakili wa Serikali Mwandamizi Renatus alidai kuwa awali wastakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa matatu hivyo walikubaliana kuliondoa shtaka la kwanza la kupanga genge la uhalifu na shtaka la tatu ni la utakatishaji wa fedha na shtaka la pili la wizi limebaki.Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai 30, mwaka huu katika Uwanja wa N…

Tundu Lissu aomba msaada kwa mawakili wa kimataifa kuhusu haki zake

Image
Mwansiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu kwa sasa anazungumza na mawakili wa kimataifa ili kupigania kile alichokielezea kama haki zake kabla ya kurudi nyumbani, limeripoti gazeti la The Citizen nchini Tanzania

Loading... Bwana Lissu, ambaye kwa sasa yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu alipigwa risasi mara nyingi mjini Dodoma yapata miaka miwili iliyopita , na sasa anapanga kurejea nyumbani.

Septemba 7, 2017, Bwana Lissu alishambuliwa kwa silaha na watu wasiojulikana nje ya makazi yake Dodoma.

"Nilipigwa risasi ndani ya makazi rasmi ya serikali kwasababu nilikuwa nahudhuria viako vya bunge. Lakini hakuna uchunguzi wa maana uliofanyika hadi sasa. Nilinyimwa matibabu nje ya nchi kama mbunge. Nilinyang'anywa kiti changu cha ubunge na bado mahakama zilininyima haki ya kuwasilisha kesi mahakamani ,"alieleza Bwana Lissu nakuongeza kuwa mawakili wataangalia jinsi hili linalindwa na sheria za kimataifa.

Lissu anaripotiwa kuwasiliana na kuwasilisna kampuni ya sheria …

Magufuli Amnyooshea Kidole Mwele Malecela Asema Alitumiwa na Mabeberu Kutangaza Ugonjwa 'Hewa' wa Zika

Image
Akielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.
Loading...
Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!

Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.

'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.

Dr. Mwele Malecela Afunguka "Asiyekuumba, Kukuumbua Hawezi"

Image
Aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI Bi.Mwele malecela ameposti katika akaunti yake ya twitter maneno haya. Nadhani huu ni mrejesho baada ya tamko la Mwenye nyumba kuwa Daktari Mwele malecela alikua anatumika na MABEBERU.

Loading...

Mjadala Juu Ya Taarifa Mpya Ya Ulaji Wa Nyama

Image
Ulaji nyama kupita kiasi umetajwa kuwa chanzo cha saratani ya utumbo. Shirika la Kimataifa linalofanya utafiti wa saratani liligonga vichwa vya habari wakati iliposema kuwa nyama husababisha saratani. Pia ilisema kuwa nyama nyekundu huenda ikasababisha magonjwa lakini hakuna ushahidi wa kutosha.

Nyeti Zake Zatoweka Kimaajabu Atembea na Mtoto wa Shehe

Image
MSHTAKIWA Faraji Ramadhani mwenye umri wa miaka 27 ameiomba  Mahakama ya Mwanzo Jijini Mbeya imruhusu ajidhamini mwenyewe kutokana na sehemu zake za siri kutoweka hivyo kupata maumivu makali anapokuwa mahabusu.
“Hakimu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa shehe, Ustadhi huyo alinionya sana kuachana na binti yake lakini sikusikia, ndio chanzo cha sehemu zangu za siri kupotea, nikiwa nyumbani natumia dawa za miti shamha kutuliza maumivu,” alisema Ramadhani mahakamani.
Kutokana na malalamiko hayo Hakimu Manase aliamuru mtuhumiwa huyo aliyefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa kompyuta akaguliwe na baada ya askari kumkagua ilibainika anachokisema ni kweli.
Hata hivyo,  Hakimu Diana Manase wa Mahakama hiyo ya Mwanzo Jijini Mbeya aligoma kumruhusu kujidhamini kwa madai akitoroka hawezi kujua wapi kwa kumpata na kumtaka avumilie kwa kuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana shehe alimuonya aachane na binti yake akakaidi, Kesi imeahirishwa hadi Septemba 27 mwaka huu.

Ujenzi Stendi Mpya Mbezi Louis wamridhisha Makonda

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo September 23 ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Stand mpya ya kisasa ya Mabasi ya Mikoani na Nchi za Jirani ya Mbezi Luis ambayo ujenzi wake umefikia 35% hadi sasa na Kumtaka Mkandarasi kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati. RC Makonda amesema ujenzi wa Stand hiyo utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 50.9 ambapo ndani yake kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo Jengo la Abiria,Utawala, Maegesho ya mabasi 500, Shopping Mall, Hotel, Maegesho ya Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo, Kituo cha Polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo. Aidha RC Makonda amemuelekeza katibu Tawala wa Mkoa huo kuunda Kamati ya kufuatilia Maslahi ya wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika miradi ya kimkakati ili kuhakikisha wanapata stahiki zao zote ikiwemo mishahara na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Darasa Kuangukiwa Wanafunzi 7 Wafariki - Video

Image
Wanafunzi saba wamethibitishwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya darasa la shule yao kuporomoka leo Jumatatu Septemba 23, 2019 asubuhi Nairobi nchini Kenya.

Wanafunzi kadhaa bado wamekwama ndani ya jengo hilo na shughuli za uokozi zinaendelea. Mafisa wa zima moto wa Baraza la jiji la Nairobi kwa ushirikiano na Shirika la Msalaba mwekundu wanasaidiana na wenyeji kuwaokua watoto waliokwama chini ya jengo hilo. Kamanda wa polisi George Seda na mbunge wa eneo la Dagoreti, John Kiarie, wamethibitisha kuongezeka kwa idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo.
Mkurungezi wa shule hiyo ya kibinafsi, Moses Wainaina Ndirangu, amaeiambia Runinga ya Citizen nchini Kenya kuwa jengo hilo liliathiriwa na ujenzi wa bomba la maji taka karibu unaoendelea karibu na hapo. Baadhi ya wanafunzi wanasemekana kukiimbilia makaazi ya watu walio karibu na mtaa waDagoretti, Magharibi mwa Jiji la Nairobi baada ya jengo la shule kuporomoka.

Mbosso afunguka kifo cha mzazi mwenzake Boss Martha "tulikuwa tunatafuta nyumba"

Image

VIDEO - WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI SABA WALIOCHUKUA BILIONI 1.3 | VIDEO MP4

Image

VIDEO: MAMA SAMIA ALIVYOAGA MWILI WA HAYATI MUGABE ZIMBABWE!

Image
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameungana na viongozi wa nchi mbalimbali katika kuuaga mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, katika viwanja vya Rufaro jijini Harare.

VIDEO: MREMA, KUPINGA WATU WANAOMKASHIFU RAIS MAGUFULI

Image
MWENYEKITIwa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema,  alizaliwa mwaka 1945, huko mkoani kilimanjaro katika kijiji cha Kilaracha kilichopo Moshi vijijini akiwa mzaliwa wa pili katika familia ya watoto watano ya Mzee Lyatonga Mrema. Safari ya Mrema kwenye ulingo wa siasa ilianza mnamo mwaka 1966 baada ya kujiunga na chama cha mapinduzi CCM. Miaka yake katika siasa amepata nafasi ya kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo mwalimu wa siasa katika wilaya mbalimbali nchini,Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo, na badaye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hata hivyo hakikuwepo kwenye Katiba ya nchi.
Huyo ndiyo Agustino Lyatonga mrema, mbali na kujiengua kutoka chama cha CCM na kuhamia NCCR Mageuzi na badaye TLP Mrema hajawahi kuacha kulitumikia taifa kwa kile anachoamini kuwa kinalipata taifa manufaa ya kusonga mbele kimaendeleo.

Polisi Dar ‘Yaua’ Majambazi Sugu HABARI NA VIDEO

Image
Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam mnamo tarehe 25/08/2019 majira ya tatu na nusu usiku huko maeneo ya Pugu, lilifanikiwa kukamata silaha mbili aina ya Shortgun na bastola.
Katika ufuatiliaji alikamatwa mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la OMARY ATHUMANI @ DANGA MIAKA (39), mkazi wa mkuranga ambaye pia alikuwa anatafutwa kwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha, katika mahojiano ya kina mtuhumiwa alikiri kujihusisha na matukio mbalimba ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kuwa amewahi kufungwa miaka 30 na alitoka kwa rufaa na kujiunga na kundi lingine la ujambazi.
Mtuhumiwa huyo pia alieleza kuwa kuna wenzake watatu ambao anashirikiana nao pia wamepanga wakavamie na kupora duka la M-pesa lililopo maeneo ya Pugu shuleni hivyo yuko tayari kuwapeleka Askari eneo la tukio, kikosi kazi wakiwa na mtuhumiwa waliweka mtego na ilipofika muda huo eneo la Pugu washirika wake walijitokeza toka kwenye kichaka wanakoficha silaha mara wakagundua kuwa wanafuatil…